BAADA YA AFYA YA RAIS KUZOROTA HATIMAYE AKUBALI KUJIUZULU
Afya ya Rais yazorota
WEDNESDAY , 21ST MAR , 2018
NA MWANDISHI WETU
Rais wa Myanmar Htin Kyaw amejiuzulu kulingana na taarifa iliyotolewa na ofisi yake ambapo hakuna sababu zilizotolewa ingawa kumekuwa na taarifa za kuzorota kwa afya yake katika miezi ya hivi karibuni.
Htin Kyaw mwenye umuri wa miaka 71 aliapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo 2016 baada ya ushindi katika uchuaguzi huru uliofanyika nchini humo na kumaliza utawala wa kijeshi uliodumu kwa miongo kadhaa.
Hata hivyo Rais huyo alikuwa asiye na madaraka, kwani ushindi wa kidemokrasia uliopatikana katika uchaguzi huo ukiongozwa na kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi ambaye kulingana na katiba ya nchi hiyo ambayo kifungu kiliandikwa kwa makusudi ya kumzuia kuwa Rais wa nchi hiyo kikiainisha kwamba raia wa taifa hilo ambaye ana watoto wa utaifa mwingine hawezi kuwa Rais na Kyi ana watoto wawili ambao alizaa na mume wake muingereza ambaye alifariki
Taarifa ya kujiuzulu kwa Rais Kyaw ilitolewa kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo alisema anataka kupumzika. Makamu wa Rais Myint Swe, ambaye ni generali wa zamani wa jeshi atakuwa kaimu Rais mpaka hapo Rais mpya atakapochaguliwa katika kipindi cha siku saba.
No comments: